ENTERTAINMENT

DNA: Mr Nice ni msanii mwenye historia ya pekee Afrika Mashariki



“Nice ni mkali wa wakali, Nice ni mnoma, yaani kwa historia ya muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki, Nice yupo huko juu, amefanya vitu ambavyo havijafanywa na watu wengi na kina Chameleone na ma’legend, Nice is up there,” amekiambia kipindi cha The Cruise cha EA Radio.
“Nice tumewakuta wakati bado tunahustle street tukiuza simu, Nice alikuwa ameshavuma, Nice yuko na talent sana,” ameongeza.
DNA ameendelea kumsifia Mr Nice kwa kudai kuwa akiamua anaweza kurudi vizuri kama hapo mwanzo kutokana na nyimbo zake za zamani zinaendelea kufanya vizuri kwenye nchi tofauti tofauti ikiwemo Kenya, Sudan, US na UK.
Hivi karibuni Mr Nice ameiambia Bongo5 kuwa yupo nchini Kenya akiandaa wimbo wake mpya aliomshirikisha Wyre pamoja na kufanya show katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.