Sababu za Mahusiano Mengi Kutodumu...
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini mahusiano mengi hayadumu kwa mda mrefu na hata yakidumu simoja kwa moja. Wengine huusianisha na udanganyifu wa mapenzi.
Hizi ni baadhi tu ya sababu za mahusiano mengi kutofikia mwisho.
1. Tabia Mbaya
Hizi ni tabia zisizokubaliwa na jamii ama watu wengi. Kwa hakika mahusiano mengi yanapoanza watu wengi huficha tabia zao. Lakini, kwavile tabia ni ngozi basi kamwe haziwezi dumu katika hali ya mficho. Baadae hujitokeza nakuanza kuwa changamoto za kimahusiano ambazo zinaweza pelekea kuvunjika kwa mahusiano. Mfano wa tabia hizo mbaya ni kama ulevi wakupindukia.
2. Kutojiamini
Mahusiano mengi yamekuwa yakivunjika kwa sababu ama mmoja ama wawili walio katika mahusiano hawana imani yakujitosheleza. Nidhahiri kuwa kama huna imani yakudumu kwa mahusiano ni vigumu sana kwa mtu kuekeza ama kujikabidhi moja kwa moja. Hivyo watu wengi wasio na imani na mahusiano yao huishia kufanya mambo yakawaida tu na yasiyoweza kuchochea maendeleo ya kimausiano.
3. Maamuzi
Hili ni swala lingine ambalo limekuwa likikwamisha maendeleo ya mahusiano mengi. Kuna baadhi ya watu hasa wanaume hupenda kufanya mambo yao peke yao hata kama yanawahusu wenza wao. Hili ni jambo ambalo wanawake wengi hawalifurahii. Mahusiano ni pamoja na kushirikiana na kushirikishana. Hali hii ya kutoshirikishana katika maamuzi wakati mwingine ina nafasi kubwa katika kuvuruga mahusiano.
4. Fedha
Uchumi nao umekuwa changamoto za mahusiano mengi. Wanawake wengi hupenda wanaume wenye kuweza kuwaudumia na kuwatimizia mahitaji yao. Wakati huo huo wanaume hupenda wanawake ambao angalau wapo vizuri kiuchumi ili waweze kusaidiana katika majukumu. Sasa pale inapotokea mwanamke yeye ni kuomba tu kila siku hupelekea mwanamume kumchoka na ikitokea amekutana na mwanamke mwingine mwenye utofauti kidogo basi huweza kumsahau kabisa mwenzi wake.
Lakni pia mtu akiwa kwenye mahusiano lazima awe muwaz Ili mambo yawe vzr,,,pia Mungu apewe nafasi yake
ReplyDelete