PICHA 6: MAVAZI SAHIHI KATIKA FUKWE NA MAENEO MENGINE YA KUOGELEA.
Akili ya mwanadamu huchoka baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu. Inashauriwa kuipumzisha ili kuijengea uwezo zaidi wa kiutendaji. Moja kati ya sehemu unazoweza kwenda kufanya mapumziko ni ufukweni.
Watu wengi hupendelea kutembelea fukwe mbali mbali ama kuogelea ama tu kutuliza akili zao huku wakipata upepo mwanana tokea baharini.
Katika maeneo ambapo hamna bahari watu wengi hupendelea zaidi kutembelea maeneo ya kuogelea kama sehemu ya kubadilisha mazingira ila pia kujipumzisha.
Wengi hujiuliza ni lipi vazi sahihi la kwendea na kuvaa katika fukwe ama maeneo ya kuogelea? Hii inatokana na mazoea kwa wengi kujiendea na mavazi yasiyo rasmi kwa Mfano vazi la suti, ama nguo nzito.
Jibu ni rahisi sana. Mtu anaweza kwenda na vazi lolote katika sehemu hizo kadri apendavyo. Ila, inashauriwa kwenda katika mavasi mepesi na yasiyo na joto kali bila kujali unadhamiria kuogelea ama la.Hii itakusaidia kupata hewa safi, kuwa huru na kukufanya mwenye uchangamfu.
Watu wengi hasa mamisi wamekuwa wakionesha yapi ni mavazi sahihi kuvaliwa katika fukwe ama sehemu za kuogelea. Mavazi hayo ni kama bukta fupi, magauni mepesi nk.
TAZAMA PICHA MBALI MBALI HAPA CHINI ZA MAVAZI SAHIHI KATIKA FUKWE AMA MAENEO YA KUOGELEA.
0 comments:
Post a Comment