Mara nyingi huwa tunazungumzia zaidi mambo ambayo wanawake wengi hupenda kufanyiwa na wanaume. Kwa leo ningependa kukufahamisha baadhi ya mambo ambayo mara nyingi wanaume nao hupendelea kufanyiwa na wenza wao (wanawake) japokuwa wanaeza kamwe wasikuambie.
Hakuna mtu asiyependa kusifiwa katika mambo anayoyafanya lakini kuomba kusifiwa si jambo la kawaida. Kunatofauti kubwa kati ya wanawake na wanaume. Tutumie mfano mdogo wa mitandao ya kijamii; ni rahisi kwa mwanamke akisambaza picha kuona watu wengi (wanaume kwa wanawake) wakimsifia aidha muonekano ama uzuri wa picha. Swala hili huwa si la kawaida kwa wanaume wanaposambaza picha zao ama makala zao.
Hii haimaanishi kuwa wanaume hawapendi kusifiwa, la hasha. Fikiri juu ya hilo na pale mwenza wako anaposambaza picha ama ujumbe wake wowote kuwa wakwanza kumpongeza; Umependeza mpenzi; kwa sababu huwa wanaume wanapoambiwa hivyo hujisikia faraja sana na wewe ndiye mtu sahihi wa kumpa hiyo faraja mpenzi wako.
Waaume wengi hupenda kuona wakiombwa ushauri na wenza wao hata kwa mambo madogo. Mwanamke kumwomba mwanaume ushauri anapotaka kufanya jambo humwongezea mwanaume imani na fikra za kwamba yeye ni mtu wa muhimu katika maisha yako. Anza kufanya hivyo katika mahusiano yako na uone mabadiliko.
Kushirikishana katika mawazo ni jambo la msingi katika mahusiano. Wanaume wengi hujisikia wa maana na muhimu sana katika maisha ya wanawake pale wanaposhirikishwa mambo mbali mbali na wenza wao katika lugha mubashara.
Badala ya kumwambia mwenza wako "kwanini umefanya hivi...." waeza mwambia "mpenzi wangu nashukuru kwa......ila unaonaje ingekuwa......." Kwa namna yoyote mwanamke amshirikishe mwanaume kuhusu fikra zake na amshirikishe katika lugha iliyo jawa na mahaba.
Swala hili si la kimapenzi tu bali hata kidini na kijamii tunaimizwa kusaidiana katika mambo mbali mbali. Katika mahusiano wanaume wengi huitaji kuona wenza wao wanawasaidia japo kuwa daima sio wasemaji. Kama mmwanamke hakikisha unajenga ukaribu kwa mwenza wako na katika matatizo yake umpe msaada wa karibu ama kifikra ama kifedha. Ni katika kufanya hayo unaweza ongeza upendo kwake na mkaweza kufika mbali kuliko pale inapokuwa shida/matatizo yake ni ya kwake peke yake.
Wanaume wengi hujisikia wenye thamani kubwa kwa wenza wao hasa pale mpenzi wake anapomtumia ujumbe wa ahsubui 'Goodmorning love....' Sababu ni kwamba meseji hiyo huwa inampa ishara mwanaume kuwa yeye ni sehemu ya msingi katika maisha yako na ametawala katika fikra zako.
Wanaume hupenda sana kupokea zawadi kutoka kwa wanawake wao ijapokuwa daima hawawekagi hayo bayana. Zawadi hatakama ni ndogo ni muhimu katika kahusiano kwani ni ishara ya upendo lakini zaidi zawadi ni kielelezo cha namna unavyomkumbuka mtu flani katika maisha yako ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment