INTERNATIONAL NEWS

AFRIKA KUSINI: NAIBU RAISI AZINDUA KONDOM BUNGENI


Naibu wa rais nchini Afrika Kusini alipokuwa akijibu maswali juu ya mkakati wa serikali kuhusiana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi  bungeni aliweza kutambulisha aina mpya ya Kondomu iitwayo Max katika mionekano na ladha tofauti tofauti ikiwemo ladha ya Apple na  machungwa. Sifa ya nyongeza kupitia kondomu hizo ni kutokuwa na makelele, aliwaambia wabunge.

Cyril Ramaphosa alielezea kwamba mipira hiyo ya kondomu ilitengezwa kufuatia malalamishi kwamba kondomu za serikali zilikuwa zina harufu mbaya na kelele.

Tangazo hilo la Ramaphosa lilizua hasira na tabasamu kutoka wanachama wa ANC na kelele kutoka kwa upinzani wa chama cha EFF huku baadhi ya wanachama wake wakisema ''mpatie Zuma hizo''.

Matamshi hayo ya wanachama wa EFF yanatoka miaka 10 iliopita wakati bwana Zuma alipokiri kwamba katika kesi yake ya ubakaji ,alifanya mapenzi bila kutumia mipira ya kondomu na mwanamke aliyekuwa na virusi vya HIV.

Aliondolewa mashtaka hayo lakini kukiri kwake kulizua mshangao mkubwa nchini humo ambapo takribani watu milion saba wana virusi.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.