SPORTS

VITA KATI YA MAN CITY NA MAN UTD LEO


Leo kujulikana fundi nani na kibarua ni nani. Ni katika mechi ya Man City na Man United ambapo vilabu hivyo viwili maarufu tokea jiji la Manchester vitakutana uso kwa uso.

Ikumbukwe kuwa Jose Mourinho ameshakutana na Pep Guardiola mara 16 katika vilabu mbali mbali na Mourinho ameshinda mechi 3 huku Guardiola akishinda mechi 7 na sare ya mechi 6.

Tukiongozwa na historia hiyo ya kuoneshana ubabe tunaweza tabiri mazuri kwa Man City na mabaya kwa Man Utd.

Lakini waswahili husema mpira huwa unadanda na lolote laweza tokea. Timu zote mbili zinaonekana kuwa na hari kubwa ya kukichukua kikombe msimu huu wa 2016/17 na mpaka sasa timu zote zimelingana kwa pointi.

Endelea kutembelea Page yetu kupata updates na dondoo zaidi juu ya mechi hiyo inayosubiriwa na wengi siku ya leo.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.