LIFESTYLE

HIZI HAPA BAADHI YA SABABU ZINAZOMFANYA OBAMA KUONEKANA KIONGOZI BORA .....


Rais Barack Obama ni Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya kiafrika (African American) kutawala taifa hilo. Lifestyle ya maisha yake ndiyo inayompa sifa kama kiongozi rais huyo.  Rais Obama ni mwanasheria kitaaluma na alikuwa Muhadhiri akifundisha somo la sheria ya katiba katika chuo kikuu cha Chicago shule ya sheria kuwanzia 1992 - 2008. 

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo huvifanya na humfanya kupata sifa. 

Uongeaji wake;- kama mwanasiasa Obama hutoa sauti nzito na isiyotetemeka yani Loud and clear. Katika mikutano yake na hata katika mazungumzo mbali mbali anayoyafanya kama Rais. hii huashiria uasilia katika maamuzi yake na pia huashiria utekelezekaji wa vitu anavyo visema ama kuahidi.

Obama kupitia video mbali mbali ama kwa wale walioweza kumuona live basi lazima watakiri kua ni mtu wa ucheshi na utani mwingi sio tu kwa familia yake bali hata viongozi wanaomfata kidaraja na dunia kwa ujumla.

Obama ni rais anayependa micheza na burudani kwa ujumla kuna baadhi ya videos tumemshuhudia akicheza muziki, mpira wa kikapu na hata mpira wa miguu.

Ni mtu wa kuthubutu na nivigumu sana kwake kukata tamaa, kwa wasio fahamu Rais Barack alishawahi kugombea uongozi mwaka 2000 nchini marekani na akashindwa lakini hakukata tamaa aligombea awamu nyingine na kushinda.

Ni kiongozi mpenda demokrasia na hupenda sana kuona haki ikitendeka Rais Obama kupitia hotuba zake amekua mstari wa mbele kuhimiza viongozi wa Africa kufata misingi ya demokrasia hii inatokana na chaguzi nyingi za marais wa Africa na ngazi zingine zimekuwa zikigubikwa na tuhuma mbali mbali kuhusu michakato ya uchaguzi.

Unaweza ukamuita masta wa kuongea kwa vitendo:- Ni Rais anayependa kutumia body language  katika hotuba zake hii inasaidia kuonesha kuwa anajua anacho kizungumza na hii staili hata wanafunzi wa vyuoni huwapa sifa mbele ya Wahadhiri wao pindi wakiwasilisha kazi zao kwa kuonge katika majukwaa ya madarasa yao.

Ni Rais anayependa watoto. ni nadra sana kumkuta Rais huyu akiwapita watoto bila kuwatania au kuwachekesha. wakati baadhi ya viongozi huwasalimia watoto pindi za uchaguzi. kitu ambacho huwafanya wapiga kura wao waamini wanafanya hivyo kwa nia ya kupata nafasi wanazo wania. Rais pia hujibu barua za watoto wanazo muandikia baadhi ya watoto hao ni Miss Flint Mari msichana wa miaka 8 huko marekani na Christopher Kule mvulana aliyejibiwa barua na Rais akiwa na miaka 10 kutoka nchini Uganda Kasese.
Staili yake ya kuvaa na kukunja shati la mikono mirefu nayo imempa sifa sana duniani ambapo watu wengi hutafsiri utayari wa kiongozi huyo kufanya kazi na kutumikia watu.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.