SPORTS

MWANASOKA WA LEO......


Leo niko hapa kukudondoshea baadhi ya mambo kuhusu mwanasoka wako wa leo. Huyu si mwingine bali ni Lionel Messi.

Nikwamuda sasa pamekuwa na gumzo katika mitandao mbali mbali ya kijamii na vyombo vya habari kama Lionel Messi ni mwanadamu wakawaida. Hii inatokana na uwezo wake mkubwa pamoja na miujiza yake yakisoka anapokuwa uwanjani katika zama hizi za soka.

Nikujuze tu kama hukuwa unafahamu kwa sasa Lionel Messi amefanikiwa kufikisha magoli 25 katika ligi ya soka ya Hispania ukiwa ni msimu wa tisa mfululizo toka 2009/2010 ambapo alikuwa na magoli 34.

Katika msimu huu Lionel Messi ana idadi ya magoli 25 akiwa amemtangulia Christiano Ronaldo wa R. Madrid aliyefikisha magoli 22 hapo jana baada ya kuifungia timu yake magoli 4 dhidi ya Girona

Kwasababu ya ushindani Lionel Messi anaoupata tokea kwa mpinzani wake 'Ronaldo' gumzo kuu kwa sasa ni nani kuibuka Mfungaji bora wa ligi "Pichichi" msimu huu.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.