GOSSIP

Lulu afunguka haya kwawale wanao mtukana kwenye mitandao ya kijamii

Kwenye mitandao ya kijamii sikuhizi sio kitu cha ajabu kwa staa kuvamiwa na mtu ambaye hata hawafaamiani na kuanza kushushiwa matusi ya nguoni na hata yasio ya nguoni.
Watumiaji wengi wa kwenye mitandao wasio jua umuhimu wa kwenye mitandao na picha wanayo jijengea kwenye mitandao hiyo wamekuwa wakifany akila wajihisicho pasipo kujua wanaharibu picha yao kwa jamii kubwa inayo wafatilia kila siku.
Kwa muigizaji wa Bongo movie, Elizabeth Michael aka Lulu, yeye alibahatika kufanya mahojiano na gazeti la Mtanzania na alipoulizwa anazungumziaje skendo zinazokuandama katika mitandao ya kijamii na wale ambao hukushushia matusi.
Lulu alisema “Nachukulia kama changamoto tu katika kazi kwani kuna mambo mengine nahusishwa nayo ila siyajui. Ila ninachojua, hao wanaonitukana ndiyo haohao mashabiki wangu, sema wanajibalaguza tu lakini moyoni wananikubali“.
Pia akizidi kuweka wazi kwakusema “Kama binti napenda maisha mazuri ndiyo maana najituma ili niweze kufanikiwa. Kama nilivyosema huwa sipendi uzushi na ugomvi, ndiyo maana ninapozushiwa au kutukanwa mara nyingi huwa nanyamaza kwa kuwa sipendi malumbano na watu. Napenda amani.


About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.