LOCAL NEWS

Mwili wa Marehem Joseph Senga wa agwa leo.......Na hizi ni baadhi ya picha na matukio.


Moja ya headline iliyotawala July 28 2016 katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ilikuwa ni pamoja na hii ya kutokea nchini India iliyohusu kifo cha mpiga picha wa Gazeri la Tanzania Daima Joseph Senga aliyefariki akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo. 

Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea  September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Leo July 30 2016 mwili wa marehemu Joseph Senga tayari umewasili nchini ukitokea India, ambapo Waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye aliungana na baadhi ya watanzania wakiwemo wapiga picha wenzake wa kutokea vyombo mbalimbali vya habari.

uhai 
                                              Marehemu Joseph Senga enzi za uhai wake

WhatsApp-Image-20160730 (4)

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.