Gai amuomba Machar kurejea nyumbani kujianda kwa uchaguzi
Makamu wa rais wa kwanza wa Sudan Kusini Taban Deng Gai, amemlaumu kiongozi wa waasi na aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Riek Machar, kwa kuhujumu amani katika taifa hilo changa zaidi duniani kwa nia ya kunyakuwa madaraka kutoka kwa rais Salva Kiir.
Bwana Gai amemshauri mtangulizi wake Machar ambaye yuko mafichoni akimtaka arejee nyumbani na ajiandae kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka wa 2018.
Gai aliyasema hayo mjini Nairobi wakati alipowasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Salva Kiir kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .
Alikuwa mshirika wa bwana Machar lakini akakata uhusiano naye wakati kulizuka ghasia mpya katika taifa hilo jipya zaidi barani Afrika
0 comments:
Post a Comment