Mapema Jumatano ya wiki hii wakifuata muongozo wa Jaji huko nchini Brazili, Polisi walikamata paspoti za waogeleaji maarufu toka nchini Marekani, Rylan Lotche na James Feigene baada ya kuripotiwa kwa tukio la kuporwa kwa waogeleaji hao katika michezo ya olimpiki inayoendelea nchini Brazili lililotokea siku ya Jumapili.
Wakielezea kutokea kwa tukio hilo waogeleaji hao walisema, siku ya tukio walikua katika tax na walitokea watu waliojifanya maafisa polisi huku wakiwanyooshea bunduki na ndipo tukio hilo la uporaji lilipotokea.
Kama ilivyoelezwa na kamati ya mashindano hayo ya Olimpiki sababu ya kumatwa paspoti hizo nipamoja nakuruhusu kuendelea kwa taratibu za kipelelezi dhidi ya tukio hilo bila kuruhusu wahusika watukio hilo kurejea majumbani kwao.
Akizungumza na CNN mwanasheria wa Lochte amesema Lotchte amekwisharejea nchini Marekani.
Judge issues search warrants, seizure of passports for 2 US swimmers, including Ryan Lochte, around alleged robbery. https://t.co/W1UoF46mQW— CNN Breaking News (@cnnbrk) August 17, 2016
0 comments:
Post a Comment