ENTERTAINMENT

RUDY GIULIANI: "SHOO YA BEYONCE VMA 2016 NI AIBU"

Ikiwa ni siku chache tuu zimepita baada ya kutolewa kwa tuzo za VMA 2016 ambapo mwanadada Beyonce alifanya vyema baada ya kuongoza na kujinyakulia tuzo nyingi zaidi ya washiriki wote. Hii ni kwa mara ya pili kwa Rudy Giuliani (meya wa zamani wa New York City) kumuandama mwanamziki Beyonce tokea nchini Marekani.

Baadhi ya tuzo alizopata Beyonce ni Tuzo ya Video Bora ya Mwaka-Formation, Video Bora ya Mwanadada-Hold Up, Video Bora ya Pop-Formation na zinginezo.

Ni katika tamasha hilo la ugawaji tuzo ambapo mwanadada Beyonce alipata nafasi ya kutumbuiza kwa dakika kumi na tano. Kupitia mitandao mingi ya kijamiii hasa Twitter wengi wameonekana kumpongeza mwanadada huyo na kusema hakika nimwimbaji bora na pia mtumbuizaji bora.

Ni dakika 15 stegini za Beyonce zilizozuwa kizaazaa baada ya kutumbuiza katika namna inayotuma ujumbe hasa kwa wale walionaubaguzi wa watu weusi nchini Marekani. Katika tamasha hilo Beyonce alipokuwa akiingia watumbuizaji wake 16 walionekana kuanguka chini mmoja baada ya mwingine kama ishara ama picha inayosadifu mauwaji ya watu wenye ngozi nyeusi huku pakitandwa na mwanga mwekundu. Katika dakika izo 15 za utumbuizaji Beyonce alifanya tamasha kwa kupiga wimbo wake uitwao "Pray You Catch Me".

Pia katika tamasha hilo Beyonce aliudhuria na mama wa nne wa waathirika wa tukio la mauaji yaliyofanywa na polisi nchini humo na kupelekea vifo vilivyopelekea kuanzishwa kwa movement ijulikanayo kama Blacks Lives Matter.

Akijibu nakuita niyaaibu show ya Beyonce, Rudy Giuliani alisema amesaidia kuokowa maisha ya watu wenye ngozi nyeusi wengi zaidi ya waliokuwa jukwaani katika utumbuizaji na Beyonce.

HII HAPA VIDEO YA RUDY GIULIANI AKIIZUNGUMZIA PERFOMANCE YA BEYONCE

 
HII HAPA VIDEO YA BEYONCE AKITUMBUIZA... 



About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.