LOCAL NEWS

SIMANZI: KIFO CHA ABOUD JUMBE MWINYI

 
Aliyekuwa makamo wa kwanza wa Rais wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania (1972-1984) Mh. Aboud Jumbe amefariki leo tarehe 14/08/2016 jijini Dar es Salaam. Aboud Jumbe aliwai pia kuwa Rais wa Zanzibar wa awamu ya pili na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Taarifa rasmi juu ya kifo chake imetolewa na Raisi wa sasa wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed. Raisi wa sasa wa Zanzibari amesema kuwa marehemu atazikwa kesho (15/08/2016) nyumbani kwake Unguja kwakufuata wasia alioutoa marehemu kipindi cha Uhai wake.

Aidha Raisi Mohammed Ali ametangaza siku saba za maombolezo katika kutambua mchango wa marehemu. Katika kipindi chote cha maombolezo bendera zitakuwa zikipeperuka nusu mlingoti.


Raisi wa Tanzania Dkt. Magufuli amemtumia salamu za rambi rambi raisi wa sasa wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu akitambua kuwa Aboud Jumbe alikuwa mtu muhimu katika taifa na Zanzibar pia hasa ikikumbukwa aliwai shiriki katika kuipigania Tanzania, kutetea umoja na amani tuliyonayo hivi sasa.

 



About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.