LIFESTYLE

KWANINI WANASIASA NA WANASHERIA HUPENDA VALIA TAI NYEKUNDU?


Hichi ni kitu ambacho wengi wamekuwa ama wakijiuliza ama kushangaa, Ni nini siri ya vazi la tai nyekundu?

Vazi la tai nyekundu limekuwa likivaliwa mara kwa mara na wanasiasa, wanasheria, na wakati mwingine watu wa kawaida. Lakini wengi hawajawai ifahamu siri ya vazi hilo.

Tai nyekundu imekuwa ikitafsiriwa kwa namna mbalimbali katika maeneo mbalimbali na vipindi mbali mbali. Jamii ya waafrika waliowengi wamekuwa wakitafsiri rangi nyekundu katika uhusiano na nguvu za giza ama hali ya hatari.

Wakati huo huo jamii iliyokubwa ya watu wa china wao huusianisha rangi nyekundu na mambo mema na hivyo basi hata pale mtu anapodhamiria kumpongeza mwenziye hutumia baasha za rangi nyekundu.

Kama ilivyo katika nchi zingine hapa nchini tumekuwa tukishuhudia viongozi mbali mbali wakiwa katika vazi la tai nyekundu pamoja na wanasheria. Hii ni alama ya ushindi. Mara kwa mara viongozi wanapoingia madarakani ndipo kipindi hasa ambacho huanza vaa vazi hilo. Kwa wanasheria wao huanza kulivaa hasa pale wanapoapishwa kama mawakili.

Kwasababu hizi basi wewe mpenzi wa vazi la tai nyekundu jiulize kabla hujajiweka katika vazi hilo nini hasa tafsiri yako juu ya vazi hilo? Pili, Je iliyotafsiri yako ndiyo tafsiri ya wengi?


About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.