INTERNATIONAL NEWS

UK: WASICHANA WENGI HAWANA FURAHA KULINGANISHWA NA WAVULANA


Ripoti ya tasisi moja inayojihusisha na maswala ya watoto imetowa ripoti yake hivi karibuni huku ikionesha asilimia za wasichana wasionafuraha kuongezeka kwa kasi ikilinganishwa na wavulana wa umri kati ya miaka 10-15 huko nchini Uingereza.

14%  ya watoto wameripotiwa kutokuwa na amani kabisa kuhusiana na maisha yao wakati 34% hawana amani kutokana na mionekano yao.

Kwakushirikiana na watafiti toka Chuo Kikuu cha York, taasisi inayojihusisha na maswala ya watoto imepitia makazi 40,000 katika ukusanyaji data na matokeo ya utafiti wao unaonesha kunaongezeko la asilimia 3 katika idadi ya wasichana wenye umri kati ya 10-15 wasionafuraha. Takwimu za wanaume zimeendelea kubaki vile vile kama ilivyokuwa mwaka 2009-2010.

Sababu zinazousiuanishwa na matokeo hayo ni pamoja na mitandao ya kijamii na hali ngumu ya kiuchumi. Lucy Capron tokea taasisi inayojiusisha na maswala ya watopto amesema hakika hili si swala tu lakuliusianisha na homon ila ni swala la msingi na inabidi lijadiliwe.

Megan 12, Natalia 15, Caitllyn 12 walipohojiwa na BBC Radio 5 walisema kuwa wakati mwingine wakitizama mitandao ya kijamii wanaona marafiki zao na watu wengine mastaa wakipost picha zao kama wakamilifu na wazuri zaidi yao. Hakika si mionekano yao ya kweli lakini inakera wakati mwingine.

Miss Capron tokea taasisi inayojishughulisha na maswala ya watoto alisema watoto wakike ndio waathirika wakubwa wa tatizo na hii hutokana na wao kupenda kutumia muda wao mwingi zaidi katika mitandao ya kijamii zaidi ya watoto wakiume. Alisema hii inaweza kuchangia athari kubwa zaidi katika afya ya ubongo.

Taasisi nyingine huko nchini Uingereza imetowa ushahidi wa sababu ya watoto wengi wa kike wenye umri kati ya miaka 10-15 kutokuwa na furaha nikutokana na mionekano yao. Watoto wengi wa kike wamekuwa hasa katika mashule wakisikika kuchukia baadhi ya sehemu za miili yao ama kuwachukia watu wenye miili minene. Wengine wamekuwa wakijichukia wenyewe kwasababu ya miili minene.

 Based on BBC News 31/08/2016
.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.