INTERNATIONAL NEWS

ZOEZI LA UPIGAJI KURA ZAMBIA LAKAMILIKA.......

 
Uchaguzi mkuu wa Raisi na wabunge nchini Zambia umekamilika salama salmini huku wagombea urais wenye mchuano mkali zaidi ndugu Hakainde Hichilema wa chama chaupinzani (UPND) na raisi wa sasa Edgar Lungu (PF) kila mmoja akiwa  na matumaini makubwa yakuibuka kidedea.

Taarifa kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi huo toka nchi za Ulaya wameonesha kufurahishwa na mwenendo wa zoezi zima la upigaji wa kura. Cecile Kyenge (Msimamizi mkuu) kutoka Ulaya alisema watu wengi walijitokeza kupiga kura jambo ambalo linathibitisha kuongezeka kwa uelewa wa wananchi wa Zambia hasa juu ya umuhimu wa uchaguzi.

Ikumbukwe kuwa raisi wa sasa Mh. Edgar Lungu alipokea madaraka kama raisi wa Zambia Januari mwaka 2015 kufuatia kifo cha aliyekuwa raisi kwa kipindi hicho.

Zoezi zima la kuhesabu kura linatarajiwa kuanza mapema kesho na mshindi wa urais atatangazwa siku ya Jumamosi. Endapo kinara wa uchaguzi huo hatofikisha  50% basi zoezi la uchaguzi wa atakaekuwa raisi wa nchi hiyo itabidi lirudiwe ndani ya siku 37 kwa mujibu wa sheria za nchi.


About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.