SPORTS

Lionel Messi: Mechi dhidi ya Chelsea ilikuwa ni ngumu


Mchezaji Lionel Messi wa Barcelona na kepteni wa Argentina jana aliweza kuisaidia timu yake ya Barcelona kutinga katika hatua ya robo fainali UCL. Safari ya ushindi ilianzishwa na  Messi 3' baadae Ousmane Dembele 20' na goli la tatu lilipatikana kupitia kwa Messi 63'.


Mechi kati ya Chelsea na Barcelona hapo jana ilimalizika kwa matokeo ya 3-0. Pamoja na kuisaidia Barcelona kupata ushindi, mchezaji Lionel Messi sasa amefikisha magoli 100 katika michuano hiyo ya barani ulaya (UCL). Kwa mujibu wa takwimu Barcelona ilitawala kwa 56% mchezo mbele ya Chelsea waliokuwa na 44%.

Akihojiwa na vyombo vya habari baada ya mtanange huo Messi alikiri kuwa mchezo ulikuwa mgumu ila walicheza kwa bidii zote nakuweza kupata ushindi.

BOFYA HAPA CHINI KUTIZAMA VIDEO

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.