SPORTS

MZIMU WA KUPOTEZA VIKOMBE WAZIDI KUIANDAMA MANCHESTER UNITED


Ni tangu mwaka 1958 kwa mara ya kwanza klabu ya Sevilla imfanikiwa kufuzu katika hatua ya robo fainali UCL baada ya kuitandika Manchester United kwa goli 2-1. Magoli ya Sevilla yalitiwa kimyani na mchezaji Ben Yedder 74' 78' huku goli pekee la kufutia machozi kwa Man United likipatikana kupitia Lukaku 84'.

Kwa matokeo hayo safari ya Manchester United imeishia hapo UCL nakufanya mwendelezo wa safari ya Sevilla kwenda kuungana na Real Madrid na Manchester City ambao walikwisha tinga hatua ya robo fainali.

Basi wacha nikujuze mambo kadhaa kupitia mtanange huo kati ya Man United na Sevilla:
-Tangu wapokee kichapo cha 10-2 toka kwa Real Madrid 1958, jana ndio Sevilla imeweza kusonga mbele nakuingia hatua ya robo fainali UCL.
-Ben Yedder ambaye jana aliweza kuifanya Sevilla kusimama kifua mbele sasa amefikisha magoli saba msimu huu UCL.
-Tangu Sir Alex Ferguson aondoke Manchester United, hii ndio mechi ya kwanza Man United katika michuano ya UEFA kupoteza akiwa nyumbani.


About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.