INTERNATIONAL NEWS

PROF. STEPHEN HAWKING: BINADAMU ALIYEKUWA NA AKILI KUBWA ZAMA HIZI


Naaaaaaaam! Nani mwingine basi?
Haimaanishi watu wengine wote tunaowafahamu hawana akili nyingi kuliko alivyokuwa Stephen Hawking La hashaa,  Prof. Stephen katika kipindi chote cha uhai wake aliweza kuthibitisha kuwa na uwezo mkubwa wa fikra.

Najua kwa wataalamu na wanafunzi wa sayansi ni rahisi kumfahamu mtu huyu lakini kwa jamii nyingine iliyokubwa yawezekana hawajawai hata kumsikia mtu huyu.Nikiwa kama mwanataaluma niko hapa japo kukufahamisha kwa ufupi kuhusu maisha ya Prof. Stephen Hawking.

Profesa alizaliwa mwaka 1942 tarehe 8 huko Oxford, Uingereza na alijiunga na masomo St Alban's huko London kuanzia mwaka 1953-1958. Mwaka 1959 Profesa alijiunga na Chuo Kikuu cha Oxford akifanya masomo ya fizikia (Physics) na kuhitimu masomo yake 1962 akipewa Shahada ya heshima katika masomo ya sayansi.


Akiwa na umri wa miaka 21 Stephen alifanyiwa uchunguzi wa mwili wake na kugundulika kuwa na ugonjwa uitwao Lou Gehrig's ambao husababisha neva zinazoiongoza misuli kutofanya kazi tena. Nikwamujibu wa madaktari Stephen hakutarajiwa kuishi kwa zaidi ya miezi 14 tokea agundulike kuwa na ugonjwa huo.

Waswahili husema Mungu si Juma wala Athumani Stephen alifanikiwa kuishi kwamiaka mingi zaidi mpaka uzee ulipomkuta ambapo amefariki akiwa na umri wa miaka 76.


Katika maisha yake ya kifamilia, Stephen alibahatika kuwa na watoto watatu (Robert,1967, Lucy,1970 na Timothy, 1979) na aliyekuwa mwanafunzi mwenzake na mke wake Jane Wilde aliyefunga nae ndoa mwaka 1965. Hata ivyo Stephen aliachana na mwanamke huyo mwaka 1990 na kuanza maisha mapya na Bibie Ellaine aliyekuwa mwangalizi wake kiafya (Nurse)-1995 ambaye aliishi nae kwa miaka 17.

1968 Stephen alipata nafasi yakuwa miongoni mwa  wajumbe katika Taasisi Ya Maswala Ya Unajimu (Astronomy), Cambridge. 1973 Stephen alichapisha kitabu chake cha kwanza kiitwacho "The Large Scale Structure of Space-Time kwakusirikiana na G.F.R Ellis. Mwaka 2002 pia alichapisha kitabu kingine kiitwacho The Theory of Everything: The Origin and Fate of the Universes.


Mwaka 2017 mwezi wa kumi Chuo Kikuu cha Cambridge kilifanya chapisho katika ukurasa wake wa mtandao tafiti ya Stephen ya mwaka 1965 alipokuwa akisoma masomo maalumu ya Phd 'Properties of Expanding Universes'.

Nikwamapenzi ya Mungu Profesa Stephen alitutoka tarehe13/03/2018.

May his soul rest in peace.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.