ENTERTAINMENT

Real Madrid na Liverpool zatinga Robo fainali UCL 2018


Hala Madrid. Hala Zinedine Zidane...... Yapasa kukipongeza kikochi hicho cha Real Madrid kutokana na ushindi walioupata hapo jana walipokuwa wakikiputa na Paris Saint-Germaine (PSG). Matokeo ya jana ya 1-2 yameifanya Madrid kusogea hatua mbele kwa jumla ya magoli matano huku PSG wakibaki vichwa chini wakiwa na jumla ya magoli mawili kwa mechi mbili walizocheza.

Magoli ya Real Madrid yalifungwa na Christiano Ronaldo 51' Casemiro 80' wakati goli pekee la PSG likifungwa na Edinson Cavani 71'.

Kwa upande wao vijogoo Liverpool na FCPorto wao walitoshana nguvu na kutoka suluhu ya kutokufungana. Hata hivyo Liverpool imesonga mbele kwa ushindi wa goli 5 walizozipata katika mechi ya kwanza.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.