SPORTS

Ronaldo ataondoka Madrid? kaweka wazi mazungumzo yake ya simu na Perez

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno aliyeiongoza timu hiyo kutwaa Kombe la Euro 2016katika historia Cristiano Ronaldo bado anaendelea na likizo yake na kuendelea kuuguza jeraha lake la goti, Ronaldo ambaye amewahi kuhusishwa kutaka kuihama Real Madridameweka wazi mpango wake na Real Madrid.
Ronaldo mkataba wake na Real Madrid unamalizika 2018 na miaka miwili iliyopita alikuwa anahusishwa kutaka kuihama klabu hiyo na kutimkia katika vilabu vya PSGMan United au kwenda kucheza Ligi ya Marekani MLS, Ronaldo ameweka wazi  walichozungumza kwenye simu na Rais wa Real Madrid Florentino Perez.
tumblr_naza33zF2Z1rypay0o2_1280
Ronaldo na Perez
“Nimezungumza na Rais kwenye simu lakini wakati nitakapo rudi Madrid tutaongea zaidi kuhusiana na mkataba, kuongeza mkataba ni kitu ambacho nahitaji na nimekuwa nikisema hili mara nyingi na klabu wanahitaji hivyo pia, tuliongea kwa kifupi ila kila kitu kitakuwa sawa nikirudi”
Staa huyo wa kimataifa wa Ureno kwa sasa ana umri wa miaka 31 hadi atakapomaliza mkataba wake Real Madrid 2018, atakuwa na umri wa miaka 33 hivyo wengi walikuwa wanajua kuwa msimu wa 2016/2017 huenda ukawa wa mwisho kwa staa huyo kuendelea kusalia Santiago Bernabeu kwa maana atauzwa.
STORI KUTOKA: 101greatgoals.com

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.