INTERNATIONAL NEWS

Treni ya mwendo wa kasi yazinduliwa Nigeria

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria leo ameanzisha rasmi usafiri wa treni za kisasa zilizo na uwezo wa kuendeshwa kwa mwendo wa kasi.
Mradi huo wa kwanza kwa Nigeria umeigharimu nchi hiyo dolla million $850 .Reli hizo za kisasa kwa mfumo uitwao standard gauge(SGR) zilijengwa na kampuni kutoka Uchina.
Reli hizo ambazo ni mbili kwa moja yaani moja ni ya kwenda na nyengiine ya kurudi, zinaunganisha miji ya Abuja na Kaduna ambapo treni zitaweza kusafiri kwa mwendo wa kasi ya kilomita 120 hadi 150 kwa saa.
Wakati wa ufunguzi wa leo rais Buhari mwenyewe amesafiri kwa treni hiyo hivyo kuuanzishwa mfumo huo wa usafiri wa reli kwa umma.
Nauli kutoka mji huo mkuu wa Nigeria Abuja hadi mji wa Kaduna ulioko jimbo la kazkazini mwa nchi hiyo ni dolla $1:50 pekee.

Awali mradi huo ulikumbwa na chelewa chelewa za kisiasa baada ya kunzia utawala wa Obasanjo, ukapitia utawala wa Yardua hadi utawala wa Goodluck Jonathan na ndio sasa umekamilika tayari kwa matumizi katika utawala wa rais Buhari.

Zaidi ya hayo japo ujenzi wa reli ulikamilika Disemba 2014 huku treni zenyewe zikiwasilishwa nchini Nigeria miezi 15 baadaye.
Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta Nigeria imekuwa bila mfumo wa usafiri wa reli unaofanya kazi vyema kwa miongo kadhaa sasa kwa sababu ya ufisadi wa hali ya juu uliokuwa ukiendelea wakati wa tawala zilizopita.
Usafiri unaotumika sana ni ule wa barabara , ambao umekumbwa na changamoto nyingi kutokana na ajali nyingi zinazotokea, na pia magari na vilevile barabara uharibika sana kutokana na uzito wa magari ya mizigo yanayosafiri kwa mwendo mrefu.

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.