Chelsea yaanza vyema msimu mpya ligi ya Uingereza..
Chelsea almaarufu kama The Blues chini ya kocha wao Antonio Conte wameanza msimu mpya wa ligi kuu ya nchini Uingereza kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya West Ham United.
Mabao ya Chelsea yalitiwa nyavuni na Diego Costa na Eden Hazard wakati bao la kufutia machozi la West Ham likitiwa nyavuni na James Collins.
Kupitia ushindi huo Chelsea imejinyakulia pointi tatu nakushika nafasi ya tatu baada ya Man united na Liverpool.
Mpaka sasa timu zilizopo mkiani ni pamoja na Burnley, Crystal Palace na Bournemouth zikiwa hazijaambulia hata pointi moja.
0 comments:
Post a Comment