INTERNATIONAL NEWS

Watu 133 wakamatwa na Jeshi la Polisi Zambia


Baada ya Edgar Lungu kutangazwa hapo jana kama mshindi wa kiti cha uraisi nchini Zambia wapinzani wanaomsapoti Hakainde wamepinga matokeo hayo wakidai kuligubikwa na udanganyifu katika zoezi zima laupigaji kura.

Jeshi la Polisi nchini humo limekamata watu 133 kufuatia maandamano ya wapinzani hao huko ikidaiwa maandamano hayo yalikuwa yakiwalenga waliokuwa wanamuunga mkono Edgar Lungu. Chama pinzani UNPD kimesema kitapinga matokeo hayo katika mahakama ya katiba kikiwashutumu wasimamizi wa uchaguzi huo.

Marekani imempongeza Edgar Lungu baada ya matokeo hayo yaliyomfanya kutangazwa mshindi wa uraisi nchini humo.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.