SPORTS

CHELSEA YAIBUKA KIDEDEA MBELE YA BRISTOL ROVERS


Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Chelsea almaarufu kama "The Blues" wameibuka kidedea dhidi ya Bristol Rovers kwa ushindi wa magoli matatu kwa mawili katika mashindano ya League Cup.

Batshuayi ndiye mchezaji aliyeiweka Chelsea katika nafasi nzuri kabisa nakuweza kuibuka na ushindi baada ya kuweka kimyani mabao yake mawili. Goli lingine la Chelsea liliwekwa nyavuni na mchezaji Moses.

Huu ni ushindi wa tatu mfululizo ambao Chelsea wameweza kuupata chini ya kocha wao Antonio Conte ambao waweza tumika kama kiashiria kizuri hasa katika msimu huu mpya wa ligi.

Mpaka mchezo unamalizika Chelsea wameonekana wakiongoza katkika kila kitu ikiwa ni Ball Possesion 54%, Mashuti 28 kwa 7 ya Bristol, na Kona 9 kwa 3 walizopata Brisol.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.