INTERNATIONAL NEWS

Idadi ya watu waliopoteza maisha kwa tetemeko la Ardhi nchini Italy kuongezeka


Baada ya janga la tetemeko la ardhi kuikumba nchi ya Italy imesemekana miji mitatu maarufu nchini humo imearibika kabisa. Wakati zoezi la uokoaji likiendelea imeripotiwa kuwa Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko hilo imezidi kuongezeka na kufikia 120 kama ilivyoripotiwa na Waziri Mkuu Matteo Renzi wa Italy.

Mtoto wa miaka nane ameripotiwa kuwa miongoni mwawatu waliookolewa katika ajali hiyo ya tetemeko huko nchini Italy mjini Prescara del Tronto. Danilo Dionesei mkuu wa kitengo cha uokoaji alitowa taarifa hiyo huku akisisitiza mtoto huyo mwenye jinsia ya kike alifikishwa katika hospitali ya karibu. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote juu ya afya ya mtoto huyo.

ENDELEA KUTEMBELEA SITE YETU KWA HABARI ZAIDI JUU YA TUKIO HILI.


About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.