ENTERTAINMENT

SAUTI YA DIAMOND PLATNUMZ YAWA TISHIO KWA WASANII WA MUZIKI WA BONGO...

 
Diamond Platnumz ni msanii mkubwa Tanzania na Africa kwa ujumla. Kupitia lebo yake ya 'WCB' Diamond amekuwa akichangia mafanikio ya wasanii wengi akiwemo Harmonize na Raymond. Pia kwa nafasi yake Diamond amekuwa akifanya vizuri katika soko la Afrika pia katika maswala mazima ya muziki na hivi karibuni sauti yake ilisikika katika media mbali mbali akiwa na Mafikizolo katika nyimbo aliyoshirikishwa 'Colours of Africa'.

Diamond Platnumz pia ameonekana kuwatesa kimuziki wasanii wenzake kutokana na kutokupotea kwa sauti yake katika vyombo vya habari ndani na nje ya nchi.

Majuzi tu baada ya kutolewa kwa tuzo za B.E.T Diamond aliachia kibao chake kinachokwenda kwa jina 'Kidogo' akishirikiana na wasanii kutoka Nigeria Peter and Paul. Nyimbo hiyo ilionekana kukonga nyoyo za wadau wengi na kusambaa zaidi katika mitandao mingi ya kijamii.

Kupitia lebo ya WCB Harmonize aliachia ngoma yake iitwayo 'Matatizo' katika kipindi cha karibu kabisa na nyimbo ya Diamond 'Kidogo'. Wakati nyimbo yake Harmonize ikiendelea kufanya vizuri katika vyombo mbali mbali hapa nchini ilisikika tena sauti ya Diamond Platnumz akiwa ameshirikiana na Chegge wa TMK 'Waache waoane'.

Hakika mwenye nguvu ndiye atayeishi, Janjaro alimaarufu kama Dogo Janja ametoka kuachia nyimbo yake 'KIDEBE' ambayo imekuwa ikipigwa kila mara redioni na katika luninga mbali mbali. Ukiacha mbali hoja ya kwamba KIDEBE haijafanyika katika lebo ya Wasafi, ikumbukwe Janjaro wa (TipTop) kama ilivyo pia kwa Chege  toka TMK mameneja wao wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu sana na meneja wake na Diamond Platnumz.

Hii ni changamoto kwa wasanii wa Bongo kwani zipo dalili zote za nyimbo za wasanii wengi kupoteza mwelekeo hasa katika vyombo vya habari. Stori kwa sasa si Matatizo ya Harmonize wala Waache waoane ya Chege na Diamond ila ni 'KIDEBE' na 'WATORA MARI'.

Swali Je, KIDEBE itaendelea kusikika ama itapotezwa kama nyimbo za wasanii wengine?

Kama hujapata kuisikia nyimbo nyingine toka Wasafi Records iitwayo WATORA MARI Basi tazama hapa Chini.


About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.