PICHA: HAYA HAPA MATOKEO YA MECHI ZOTE UEFA ZILIZOCHEZWA USIKU HUU..
Mechi za UEFA zilizocheza leo zilikuwa ni za kipekee kabisa ukitizama matokeo na mchuano wa kila timu. Kwa upande wa Manchester City wao hawakufanikiwa kukamilisha mechi yao kama ilivyokuwa imetarajiwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mabadiliko hayo yalipelekea mechi hiyo kuahirishwa.
Katika viwanja vingine maelfu ya mashabiki wasoka walishuhudia kikosi cha Barcelona FC kikiwaadabisha bila aibu wanamichezo wa Celtic kwa goli saba sufuri.
Magoli katika mechi hiyo yalitiwa kimyani na wafungaji wa mda wote Leonel Messi (3), Luis Suarez (2), Iniesta (1) na Neymar Jr (1).
Katika viwanja vingine Arsenal walitoshana nguvu na Paris Saint German baada yakutoka kwa sare ya moja kwa moja. Goli la Arsenal lilifungwa na Sanchez.
Bayern Munich nao hawakua vibaya baada yakuibuka na ushindi wa magoli matano kwa sufuri dhidi ya Rostov. Magoli ya Bayern yalifungwa na Lewandoski (P), Mullar, Bernat, na Kimmich.
Pongezi nyingi kwa Mashabiki wote ambao timu zao zimeibuka vifua mbele...
0 comments:
Post a Comment