SPORTS

Man City wakubali kichapo cha magoli 4-0 toka kwa Barcelona...


Kwa mara ya tano Man City wanakubali kutoka uwanjani vichwa chini mbele ya Barcelona baada ya kupokea kichapo cha Goli nne sufuri katika uwanja wa Camp Nou.

Magoli ya Barcelona yalifungwa na Neymar na mfungaji wa kila mara Leonel Messi. Katika Mechi hiyo mchezaji Neymar Jr alikosa penalti katika dakika ya 87 ila aliinua shangwe za mashabiki wa timu yake dakika mbili mbele (89) baada yakufunga goli zuri lililotokana na assist ya Leonel Messi.


Ushindi wa Barcelona unazidi kuwaweka kileleni katika kundi lao wakiwa na pointi 9 huku wakifuatiwa na Man City wakiwa na point 4 tu.


Katika mechi zingine zilizochezwa  usiku huu Paris St German wameshinda goli 3-0 dhidi ya Basel, Arsenal 6-0 Ludogorets, Celtic 0-2 Borussia M'Gladbach, Bayern Munchen 4-1 PSV, Fc Rostov 0-1 Atletico Madrid na SSC Napoli 2-3 Besiktes.

About felichismi

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.